DAR ES SALAAM.
Chama cha Madaktari nchini Tanzania
(MAT) kimewakumbusha Wananchi kuendelea kuchukua Tahadhari ya kujikinga
na ugonjwa wa corona ikiwemo kunawa mikono na maji tiririka na sabuni au
vitakasa mikono licha ya ugonjwa huo kupungua ila bado upo .
Wito huo umetoleo juzi jijini Dar es salaam na
Rais wa chama hicho Dkt Elisha Osati wakati akizungumza na waandishi wa habari
juu ya tathimini ya kitaaluma ya mwenendo wa Covid 19 ambapo amesema kuwa
ugonjwa kwa Sasa umepungua kwa kiasi kikubwa kulinganisha na hapo awali, hivyo
watu wasibweteke waendelee kuchukua tahadhari ili kuhakikisha ugonjwa unaisha
kabisa.
Akitolea mfano wa kupungua kwake Dkt Osati
amesema kuwa mwezi wanne kwa Sampuli zilizokuwa zikipelekwa maabara takribani
asilimia 90 zilikuwa Chanya (Positive) ila kwa Sasa Covid 19 Chanya
imepungua chini ya asilimia 10.
Aidha Osati amesema kuwa Wagojwa walioko
majumbani kwa matatizo ya Covid 19 au magonjwa mengine waende Hospitalini
Kupata huduma kwani Madakitari wapo tayari kuwahudumia
Kwa upande wake Rais Mteule wa Chama hicho Dkt
Shadrack Mwaibambe amesema kuwa njia mbadala zinaonyesha kuchangia
katika mapambano dhidi ya covid 19 kama anavyoeleza hapa
Comments
Post a Comment