Bunge la Bajeti laendelea kujadili hoja kamati ya ya kudumu ya Bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa LAAC
DODOMA.
Bunge la Bajeti ,mkutano wa 19 kikao cha
38 limeendelea kujadili hoja ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za serikali
za Mitaa[LAAC] kuhusu ripoti ya Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa Hesabu za
Serikali[CAG] huku serikali ikishauriwa kuanzisha chuo cha Wizi ili
kukabiliana na ubadhilifu wa mali za umma.
Wakitoa michango ya maoni mbalimbali jana Mei,28,2020 juu ya Ripoti ya CAG iliyowasilishwa Bungeni jijini
Dodoma na kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za mitaa (LAAC),Mbunge
wa Kahama mjini Mhe.Jumanne Kishimba ameshauri serikali kuanzisha
chuo cha Wizi ili kuweza kupambana na ubadhirifu wa mali za umma.
Mbunge wa Ukerewe Mhe.Joseph Mkundi amesema
kuna baadhi ya watumishi ngazi ya Halmashauri wasiokuwa waaminifu
wamekuwa wakitumia Mashine za ukusanyaji mapato (POS) kwa njia ya
udanganyifu na kusababisha halmashauri kupata hasara hivyo kuna haja ya
kuwafukuza huku Mhe.Hasma Mwilima akishauri namna ya kupata mafunzo Zaidi
Wakurugenzi wa halmashauri ili kuweza kupambana na watumishi wasiokuwa
waaminifu.
Naibu Waziri wa Kazi ,Ajira na
wenye Ulemavu,Mhe.Stella Alex Ikupa amesema serikali ya awamu ya tano
imekuwa na mchango mkubwa katika kuwezesha mikopo watu wenye ulemavu,huku Naibu
waziri Ofisi ya Rais ,utumishi wa Umma na utawala bora Dkt.Mary Mwanjelwa
ametoa pongezi kwa watumishi kufanya kazi bila kuchoka ambapo Naibu
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wazee na Watoto Godwin Mollel
akizungumzia suala la tiba asilia ni suala la kibiblia.
Naibu waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe.Agelina
Mabula amesema wizara hiyo imesogeza huduma za ardhi ngazi ya mikoa huku Naibu
Waziri wa ujenzi na Uchukuzi Elias Kwandikwa akizungumzia suala la mapato Zaidi
ya Bilioni 17 hazikwenda kwenye miradi ya maendeleo ambapo Naibu Waziri wa
Kilimo Mhe.Omary Mgumba akikiri hoja ya gharama kubwa katika miradi ya
Umwagiliaji.
Akijibu hoja ya posho ya Madiwani,Waziri wa
Ofisi ya Rais ,Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa [TAMISEMI]Seleman Jafo
amesema kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni Zaidi ya Bilioni 10 zimeshalipwa
huku Mwenyekiti wa Kamati ya hesabu za serikali za mitaa
[LAAC] Vedasto Edgar Ngombale akihitimisha hoja ya kamati akiipongeza
serikali kwa kuanza kutekeleza maagizo ya CAG.
Comments
Post a Comment