BILIONI 175.6 KULETA NEEMA YA MAJI MJINI MOROGORO


Na. Mwandishi Wetu, MOROGORO
Shilingi bilioni 175.6 kutatua changamoto ya maji mjini Morogoro ikiwa ni moja ya hatua za Serikali ya Awamu ya Tano kuwapatia wananchi huduma bora za maji safi na salama katika maeneo yote.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James akibadilishana hati ya makubaliano ya mkopo wa masharti nafuu na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa hapa nchini, Bi. Stephanie Mouen ESSOMBE, mkopo huo utawezesha Manispaa ya Morogoro kunufaika na mradi wa maji wa Bilioni 175.6
Akizungumza leo June 27, 2020 jijini Dodoma wakati wa kutiliana saini mkataba wa mkopo wa masharti nafuu kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Doto James amesema kuwa utekelezaji wa mradi huu utawezesha wakazi wapatao 722,000 kupata maji safi na salama katika mji huo.

“Kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, napenda kutoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Ufaransa  kupitia AFD kwa ushirikiano mzuri uliopo unaowezesha kutekelezwa kwa miradi mingi ya maendeleo kwa mikopo ya masharti nafuu”, alisisitiza Bw. James.

Akifafanua amesema kuwa upatikanaji wa maji utaongezeka katika mji wa Morogoro kutoka mita za ujazo 33,000 kwa siku hadi kufikia mita za ujazo 89, 000 kwa siku baada ya kukamilika kwa mradi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Prof. Kitila Mkumbo amesema kuwa utekelezaji wa mradi huo katika mji wa Morogoro utatatua changamoto ya maji kwa wakazi wake na kuchochea maendeleo.

“Miradi ya maji 1423 inatekelezwa kote nchini huku 792 imekamika na inatoa huduma kwa wananchi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli ambapo mwaka 2015 aliahidi kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji vijijini na mijini”, alisisitiza Prof. Mkumbo.

Akifafanua amesema kuwa utekelezaji wa mradi huo utoa fursa za ajira kwa watanzania na viwanda vya ndani vitaweza kunufaika kwa kuzalisha mabomba na vifaa vingine vinavyohitajika katika mradi huo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa hapa nchini, Bi. Stephanie Mouen Essombe amesema kuwa Shirika hilo litaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kutekeleza miradi ya maendeleo.

Akifafanua amesema kuwa mradi huo utawezesha wakazi wa Manispaa ya Morogoro kufikiwa na huduma ya maji safi na salama kwa asilimia 90 ifikapo mwaka 2025.

AFD imeshatoa bilioni 655 katika kipindi cha miaka 10 katika sekta ya maji hapa nchini na hivyo kuchochea maendeleo.

MWISHO

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.