Na. Mwandishi Wetu, DODOMA
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo amelitaka Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) na Taasisi ya elimu (TET) kuhakikisha utaratibu wa kufanya marejeo ulioanza kwa kidato cha sita uhusishe madarasa yote yanayotarajia kufanya mitihani ya Taifa.
Aidha, amewataka
wanafunzi kuzingatia ratiba ya masomo inayotolewa ili wasikose vipindi na hivyo
kuwafanya kuwa nyuma tofauti na wenzao pindi wakirudi shuleni.
Waziri Jafo ametoa maelekezo hayo leo
ofisini kwake wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utaratibu wa
masomo kwa njia ya runinga,redio na mitandao ya kijamii.
AMEzipongeza taasisi zote binafsi
zilizoshirikiana na serikali kuhakikisha lengo lake linatimia katika kipindi
hiki cha mpito cha ugonjwa wa Corona unaosababisha homa kali ya mapafu(COVID
19).
Akizungumzia suala la Covid 19, Waziri Jafo amependekeza kuwepo kwa wiki ya kujifukuza nchini ili
kuweza kupunguza maambukizi hayo na kufuata ushauri mbalimbali unaotolewa.
Amewataka watu kutoona aibu bali wajifukize
na kula lishe nzuri ili kuimarisha afya zao .
MWISHO
Comments
Post a Comment