Wajasiriamali jijini Dodoma waelezea hali ya biashara zao katika kipindi hiki cha Mlipuko wa Ugonjwa wa Corona
Na. Jackline Kuwanda, DODOMA
Licha ya uwepo
wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona
(COVID-19) hapa nchini, Wajasirimali wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali
hapa jijini Dodoma wameendelea kufanya shughuli zao kama kawaida huku
wakiendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo kwa kufuata maelekezo
yote ambayo yametolewa na wizara ya Afya.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti na Mtandao wa Dodoma News Blog wajasirimali hao akiwemo
Emmanuel Mazengo na Juma Athumani ambao ni wapiga picha katika bustani ya Nyerere Square wamesema
kuwa uwepo wa ugonjwa huo katika biashara yao imewaathiri kwa kiasi kikubwa
kwani idadi ya wateja waliokuwa wakifika katika eneo hilo imepungua tofauti na
ilivyokuwa hapo awali huku wengine wakisema kuwa wanaendelea kuchukua tahadhari
kama kawaida dhidi ya ugonjwa huo.
“Hali
ya uchumi imekuwa ngumu kwa wapiga picha na sisi tu peke yetu bali hata sekta
nyingine, kwasasa
unaweza kushinda bila hata kupiga picha moja, tunaona namna ambavyo vijana wetu wanahangaika hapa, sisi pia tunavyo hangaika hakuna chochote kwa upande
wetu hili janga ni kubwa’’.
Ally Gwendo ni
Mjasirimali anayejishughulisha na bidhaa za uchongaji wa vinyago yeye anasema kwa sasa kwa
wachonga vinyago hali imekuwa si nzuri ambapo kwa pindi cha nyuma hali ya
wateja ilikuwa ni kubwa lakini kwa sasa upatikanaji wa wateja umekuwa ni mgumu
kwani kipindi cha nyuma walikuwa wakitegemea wateja kutoka nje ya nchi ambao
walikuwa wakija kutalii ndani ya nchi ambao ndio walikuwa wateja wao wakubwa.
“Kabla
ya corona kulikuwa na mwitiko mkubwa kwa wateja wetu, kutokana na asilimia
sabini, themanini tulikuwa tunategemea ni
watalii kutoka njee kwa asilimia thelathini ni wateja wa ndani ya nchi,likini
kwa kipindi hiki cha corona biashara imekuwa ni ngumu’’ Gwendo.
Mtandao wa
Dodoma New Blog umezungumza na Lukas Sospeter ambaye ni Mfanyabiashara wa Duka
la nguo hapa jijini Dodoma anasaluni yake ya kike pia, amesema kwa sasa hali ya
biashara imeshuka na hiyo ni kutokana na kuibuka kwa janga hili la corona huku
akigusia zaidi kwenye biashara ya saluni za kike namna ambavyo zimeathirika
zaidi na tatizo hilo.
“Kuna changamoto na hili janga la corona kila mtu anaogopa
kiujumla biashara imekuwa haiko sawa kama alivyokuwa zamani hususani kwenye
biashara ya saluni za kike’’ Sospeter.
Naye Abel
Majiko ambaye ni mfanyabiashashara katika soko kuu la majengo ambaye amekuwa
akijihusisha na uuzaji wa majiko katika soko hilo amesema kuwa kutokana na
janga hilo la ugonjwa corona hali imekuwa mbaye katika biashara yao lakini bado
aendelea kufanya kazi kama kawaidia huku akimshukuru Rais wa Jamhuari ya
Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuwasisitiza watanza kuendelea kufanya kazi
kwa bidi licha ya uwepo wa ugonjwa huo.
“Kama
nilivyo sema awali hali ni ngumu kwasababu sisi tunategemea wateja kutoka
vijijini sasa hivi wanashindwa kuja kwasababu wanasema kuwa mjini kuna corona’’
Majiko.
Ikumbukwe kuwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Dkt. John Pombe Magufuli licha ya uwepo wa ugonjwa huo aliwahimiza watanzania
kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuijenga nchi.
“Ugonjwa
huu kamwe usiwe kigezo ama sababu ya kuacha kufanya kazi, badala yake utupe hamasa zaidi ya kuchapa kazi, kama mnavyo jionea wenyewe tangu ugonjwa huu uaze kila
nchi imekuwa ikichukua tahadhari yake wenyewe’’ Magufuli.
MWISHO
Comments
Post a Comment