DODOMA
Bodi
ya ushauri ya wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA Imeagizwa kuhakikisha kuwa
inajiendesha kibiashara pamoja na kukusanya Jumla ya tani laki moja na
elfu ishirini ya akiba ya chakula.
Kauli hiyo imetolewa Jijini Dodoma Dodoma na Waziri wa kilimo Mhe.Japhet Hasunga wakati wa uzinduzi wa bodi ya ushauri ya Wakala wa hifadhi ya taifa ya Chakula NFRA.
Kauli hiyo imetolewa Jijini Dodoma Dodoma na Waziri wa kilimo Mhe.Japhet Hasunga wakati wa uzinduzi wa bodi ya ushauri ya Wakala wa hifadhi ya taifa ya Chakula NFRA.
Waziri Hasunga amesema katika kipindi hiki cha Mavuno NFRA inapaswa kujipanga vyema namna nzuri ya kupata fedha ili iweze kuingia sokoni kwani mwaka jana haikufanya vizuri na ilinunua tani elfu tatu pekee.
‘’ili kuongeza utendaji kazi wa wakala sasa nina iagiza bodi kufanya yafuatayo jambo la kwanza ni kuhakikisha wakala wanajiendesha kibiashra bila kusahau jukumu lenu la msingi wa utoaji wa huduma kwa umma kwa hiyo sasa hivi ni kipindi cha mavuno ninaamini katika siku mbili hizi mtakazo kutana jambo kubwa mtakalo lijadili ni namna ya kupata fedha kwajili ya kupata manunuzi’’Hasunga
Mtendaji mkuu wa wakala wa taifa wa hifadhi ya chakula nchini,NFRA Milton Lupa amebainisha baadhi ya mambo waliyotekeleza ikiwa ni pamoja na kupeleka chakula mikoa ya kanda ya kati na kanda ya ziwa tani elfu tatu ili kuhimili mfumuko wa bei pamoja kupeleka chakula katika maeneo yaliyokumbwa na mafuriko hususan mkoani Lindi takriban tani 117 na
Rufiji tani 26 na kuuza kwa bei nafuu.
Aidha katika ujenzi wa vihenge vya
kuhifadhia mazao Bw.Lupa amesema umekabiliwa
na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na virusi vya Corona ambapo watumishi waliokwenda nchini
Poland imekuwa vigumu kuja nchini na waliopo
nchini imekuwa ngumu kwenda kwa ajili ya kujengewauwezo.
Mwenyekiti wa bodi ya Ushauri NFRA
Mhandisi Yustak Kangolle amezungumzia
umuhimu wa Maslahi kwa watumishi ili waweze kufanya kazi kwa kujituma huku pia akiiomba serikali kuongeza
idadi ya watumishi kwani walio wengi
wamekaimu kwa muda mrefu.

Comments
Post a Comment