DODOMA.
Waziri wa
Maji Profesa Makame Mbarawa ametaja mwarobaini wa ukamilishaji wa miradi ya
maji nchini kuwa ni force akaunti na kusisitiza kuwa hakuna mtu atakayezuia
kutumia utaratibu huo.
Akijibu hoja zilizotolewa na wabunge wakati wa mjadala wa bajeti
wa wizara hiyo Profesa MBARAWA amesema utaratibu huo kwanza unaokoa fedha,pili
unaokoa muda wa ukamilishaji wa mradi lakini pia unajengwa kwa kiwango tofauti
na awali walivyokuwa wanatumia wakandarasi.
Pamoja na mafanikio hayo Profesa MBARAWA anataja changamoto
iliyopo katika utekelezaji wa utaratibu huo kuwa ni baadhi ya watumishi wa
wizara kutoukubali.
Kwa upande wake spika wa bunge JOB NDUGAI ameunga mkono
utaratibu huo ili kuondoa ucheleweshaji wa miradi ya maji.
Utaratibu wa force akaunti kwanza unatajwa unaokoa fedha,Pili
unaokoa muda wa ukamilishaji wa mradi lakini pia unajengwa kwa kiwango tofauti
na awali walivyokuwa wanatumia wakandarasi.

Comments
Post a Comment