Na. Mwandishi wetu, MOROGORO
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, amefanya ziara mkoani Morogoro na
kumwagiza Mkandarasi, Kampuni ya State Grid, anayetekeleza Mradi wa Umeme
Vijijini, mkoani humo kumaliza kazi kwa wakati.
![]() |
| Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (mwenye ushungi), akikagua Yadi ya Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Umeme Vijijini, wilayani Gairo |
Mgalu alilazimika kufanya ziara hiyo baada ya kupokea malalamiko ya
kusuasua kwa Mradi husika ambapo aliwaagiza watendaji wa Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kumsimamia Mkandarasi
huyo ili kuhakikisha anakamilisha kazi kwa muda ulioainishwa kwenye Mkataba.
Wakati wa ziara hiyo iliyofanyika Aprili 25 mwaka huu, Naibu Waziri
alitembelea baadhi ya vijiji vya Wilaya za Gairo na Mvomero kujionea maendeleo
ya kazi husika.
Vijiji vilivyotembelewa ni Ukwamani na Nguyami (Gairo) pamoja na
Komtanga (Mvomero). Kadhalika, Naibu Waziri alitembelea Yadi ya Mkandarasi
iliyopo Gairo Mjini.
![]() |
| Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati-mwenye ushungi), akikagua kazi ya kuunganisha umeme vijijini inayoendelea katika eneo la Ukwamani, wilayani Gairo |
Naibu Waziri aliwaasa viongozi na wananchi wote kwa ujumla kuendelea
kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa Covid – 19 unaosababishwa na virusi vya
Corona huku wakiendelea kufanya shughuli zao.
Pia, aliwataka TANESCO Mkoa wa Morogoro kuhakikisha wananchi wote
wanaolipia ili kuunganishiwa umeme, wanapatiwa huduma hiyo kwa wakati.
MWISHO


Comments
Post a Comment