Mazishi ya Naibu meya Morogoro Kusimamiwa na Serikali



MOROGORO.

Mkuu wa mkoa wa morogoro Loata Ole Sanare amesema   mazishi ya aliyekuwa Naibu Meya wa manispaa ya morogoro Isihaka Sengo yatasimamiwa na serikali na kuzikwa na watu wasiozidi kumi.

Akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama mkoani humo mbele ya waandishi wa habari  sanare amesema kuwa  hakuna sababu ya kusubiri majibu   ya kitabibu kwani tayari muongozo  unaozuia uwepo wa mikusanyiko isiyo ya lazima ili kuepukana na virusi vya korona inayo pelekea homa kali ya mapafu  hivyo  ni vyema mwili huo ukahifadhiwa  aprili 28  katika makaburi ya Kibwe yaliyopo  mansipaa hiyo.bila kusubiri majibu hayo.

Hata hivyo sanare amesema baada ya kupata taarifa za kifo cha naibu meya isihaka jana serikali ilizuia mazishi kutofanyika hadi sampuli itakapochukuliwa  ili kubaini chanzo cha kifo chake baada ya kuwepo kwa utata  na kifo hicho  lakini hadi sasa   yameshindwa kupatikana  akiongeza kuwa  mwili huo utazikwa na utazikwa  na serikali majira ya saa kumi jioni.

Ikumbukwe  Aprili 27 Mganga mkuu Manispaa ya Morogoro Ikaji Rashid baada ya kufika nyumbani kwa marehemu ambapo mwili huo  ulikuwa umehifadhiwa kisha kubainisha kuwa kutokana  na utata wa kifo hicho serikali imelazimu kusitisha taratibu na mziko hadi utaraibu mwingine utakapo tangazwa.

Kwa upande wake msemaji wa Familia bwana Mwinyimbegu Yahya ambaye ni mjomba wa Marehemu amesema ndugu yao alikua anasumbuliwa na ugonjwa wa Kisukari na ilipofika Aprili 26 mwaka huu majira ya saa tatu usiku alizidiwa na kukimbizwa katika hospitali ya Chuo cha Kilimo cha Sokoine ( SUA) na ilipofika alfajiri alifariki.

Isihaka Sengo amezaliwa mwaka 1961 na hadi umauti unamkuta alikua Naibu meya manispaa ya Morogoro.

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.