HALMASHAURI WILAYANI NJOMBE YAVUKA LENGO LA MAKUSANYO

Na. Mwandishi Wetu, NJOMBE


Halmashauri ya
Wilaya ya Njombe ambayo asilimia 70 ya mapato yake inayapata kutoka kwenye mazao ya miti, imefanikiwa kuvuka tena lengo la makusanyo ya mwaka 2019/2020 katika kipindi cha robo tatu ya mwaka kwa kukusanya asilimia 108 ya mapato.

Ripoti hiyo ya makusanyo imetolewa katika kikao cha
Baraza na Mwenyekiti wa Halmashauri, Valentino Hongoli na kutolewa ufafanunuzi na Mkurugenzi, Ally Juma ambaye anasema siri ya mafanikio makubwa katika makusanyo yametokana na ongezeko la udhibiti wa mianya ya upotevu wa mapato, Matumizi ya mashine za POS pamoja na kuweka mageti zaidi ya 18 ya ukaguzi na kwamba matarajio ni kukusanya zaidi siku za usoni.

Jitihada kubwa za makusanyo ambazo zinatajwa kuchangiwa na uzalishaji mkubwa wa mbao,
viazi na mahindi unamsukuma Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri wakati akitoa salamu za serikali ambapo ameitaka Halmashauri hiyo kuanzisha kiwanda cha kuzalisha samani ili kunufaika zaidi na mazao ya misitu badala ya kuuza miti na mbao tu.

Wakibainisha sababu zilizokuwa zikichangia kuwa na upotevu mkubwa wa mapato katika
Halmashauri hiyo baadhi ya madiwani akiwemo Roida Wanderage na Shaibu Masasi wanasema kipindi cha nyuma kulikuwa na utoroshaji wa mapato na wizi wa fedha za ushuru jambo ambalo limedhibitiwa vyema na matumizi ya mashine za POS.

MWISHO

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.