BARAZA LA MADIWANI NA WANANCHI WATAHADHARISHWA DHIDI YA CORONA


Na. Nizar Mafita, KONDOA
Baraza la Madiwani la Tatu katika Halmashauri ya Mji Kondoa limefanyoka leo tarehe 29 Aprili na kupokea taarifa mbalimbali kutoka kamati za kudumu za Halmashauri. 

Kikao kilicho fanyika kwa muda mfupi ambao ni dakika 45 ikiwa ni moja ya mazingatio ya watalaam wa ya taadhari ya kuepuka maambukizi mapya ya home kali ya mapafu covod 19. 

Akizungumza na mwandishi wa habari hii Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa, Msoleni Dakawa amesema Halmashauri inaendelea kuwakumbusha wananchi kuchukua taadhari na na kuacha kukaka katika sehemu za mikusanyiko ambayo si ya lazima mfano vijiwe vya kucheza draft, viwanda vya mpira na hata vijiwe vya kahawa. 

"Janga Hili la Corona panapopatika nafasi Kama huwezi ukaungumza bila kuzungumzia Corona tunanedelea kuwatahadharisha wananchi kwa kuzingatia maelekezo ya watalamu wa Afya na viongozi mfano so vema ukaendelaa kuzurua mjini kama huna sababu za msingi ni vyema ukaa nyumbani tu” amesema.

Amesema kuwa kituo cha Afya Bereko kimechaguliwa kuwa kituo kitakacho hudumia wagonjwa wa Corona kwa Halmashauri tatu ikiwemo Halmashauri ya wilaya ya chemba, Halmashauri ya wilaya ya Kondoa na Halmashauri ya mji Kondoa.

MWISHO

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.