Na Jackline Kuwanda, Dodoma
Wazazi wenye watoto ambao
wanaugonjwa wa Selimundu (sickle cell) wameombwa kutokukata tamaa katika
kuwahudumia watoto hao kwani baadhi ya wazazi hukata tamaa kwa kuhofia kuwa ugonjwa
huo ni wa kudumu hivyo hushindwa kuwahudumia watoto vile ambavyo inavyotakiwa.
Kauli hiyo imetolewa na Mwanzilishi
wa Taasisi ya sickle Strong Children Zuhura Hasan Makuka wakati akizungumza na
Mtandao wa Dodoma News Blog ,ambapo amesema kuwa wengi huusisha ugonjwa huo pia na imani za
kishirikina na wakati mwingine husababisha mtafaruko katika familia baaina ya
wanafamilia.
Aidha,amesema lengo kubwa la Taasisi
hiyo ni kutoa elimu kwa wazazi jinsi ya kuwalea watoto hao namna ambavyo
inavyotakiwa ili waweze kuepukana na changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza
huku akileza namna ambavyo wanawasaidia watoto wanaoumwa ugonjwa huo na wako
katika hali Duni.
Makuka amesema wameendelea kutoa
elimu kwa vijana ambao bado hawana wenza kuhakikisha kuwa wanapata wenza ambao
hawana vinasaba vya selimundu, ili ikifikia wakati wa kupata mtoto, mtoto
anazaliwa akiwa hana ugonjwa huo.
Mbali hilo Zuhura ameiyasa jamii
kutokuwa na unyanyapaa kwa watoto wenye maradhi hayo kwani humuathiri mtoto anayeugua
kuwa dhaifu zaidi kutokana na maneno anayoyapata kwa jamii iliyomzunguka.
Pia, amesema wamekuwa wakitoa elimu
zaidi juu ya kukabiliana na unyanyapa wa mitaani ambao umekuwa ukijitokeza na
endapo akikutana na mtu ambaye anamnyanyapa basi ni vizuri akamsimaisha na
kumpatia elimu zaidi kuhusiana na hali hiyo.
Hatahivyo,SELIMUNDU ni ugonjwa wa
kurithi ambao hutokea baada ya mwili wa binadamu kuwa na upungufu katika umbile
la seli, ambapo hubadilika na kuwa nusu duara .
Hali
hii ya umbile la seli kufanana na mundu, ndio iliyosababisha iitwe iitwe
selimundu au kwa jina la kitaalamu sickle cell.
Ni
ugonjwa unaorithishana vizazi kwa vizazi, lakini endapo mzazi mmoja tu akiwa na
vinasaba vya ugonjwa huu basi huwa ni vigumu kusababisha mtoto kuvipata, bali
endapo wazazi wote wawili ikitokea wana vinasaba hivyo.
Comments
Post a Comment