Wafanyabiashara Soko la Samaki Feri Wasisitizwa Kunawa Mikono mara kwa mara Kuepuka Virusi vya Corona
Na. Musa Khalid, Dar es salaam.
Maafisa
Afya wa Soko la Kimataifa la Samaki Feri Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam
wameendelea kusisitiza wafanyabishara wa sokoni hapo kunawa mikono mara kwa
mara Ili kuepukana na maambukizi ya kuenea kwa Virusi vya Corona.
Wakizungumza na Mtandao wa Dodoma News jijini Dar es salaam Maafisa Afya
hao wamesema wameamua kuwahamasisha wananchi kufata taratibu na sheria
zilizotolewa na serikali katika kujikinga na maradhi hayo ya Korona.
Afisa Afya wa soko la samaki Feri, Harold
Samweli amesema kufuatia kutangazwa kwa taarifa ya uwepo wa virusi hivyo nchini
walianza kuchukua tahadhari ya kutekeleza maelekezo ya serikali.
Marry Jonathan ni Afisa afya mazingira amesema tahadhari nyingine
waliochukua ni kuweka matangazo katika soko zima ili kila mfanyabiashara pamoja
na wateja wanapoingia waweze kulisoma na kujikumbusha.
Naye Mkuu wa Soko la hilo la Kimataifa la Samaki Feri, Denis
Mrema amesema licha ya kuwapa elimu ya kunawa mikono mara kwa mara pia
wanawaelimisha kutokusogelea pasipokuwa na sababu.
Ikumbukwe mpaka sasa Virusi vya Corona vimethibitika na
kusababisha vifo kwa baadhi ya mataifa mbalimbali duniani ambapo kwa hapa
nchini kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wataalamu wa afya zaidi ya wagonjwa 14
wamethibitika kuwa na virusi hivyo hivyo tumetakiwa kuendelea kuchukua
tahadhari.
MWISHO
Comments
Post a Comment