Na. Jackline Kuwanda, DODOMA
Jamii imeshauriwa kutofumbia macho vitendo vya
ukatili wa kijinsia ambavyo vimekuwa vikijitokeza katika maeneo yao badala yake
watoe taarifa sehemu husika ili hatua stahiki zichukuliwe.
Ushauri huo umetolewa na Lazaro Leonarld
ambaye ni mwanaharakati anayehusika na masuala ya kutoa elimu
kuhusiana na vitendo vya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia wakati
akizingumza na Mtandao wa Dodoma News Blog.
Aidha, amesema kuwa watu wengi hushindwa
kusema ukweli kutokana na vitendo hivyo wakihofia ya kuwa jamii itawachukulia
tofauti na kwa hali hiyo itakuwa ni ngumu kutokomeza vitendo hivyo.
Wakati huo huo amesema kuwa wanaongoza
kufanyiwa vitendo hivyo mara nyingi wamekuwa ni watoto wa kiume na wakike
lakini wakiume wamekuwa wakifanyiwa ukatili wa kijinsia mara nyingi na wengi
wao wamekuwa wakipata madhara makubwa na ameendelea kuiasa jamii kutofumbia
macho vitendo hivyo.
Katika hatua nyingine amesema vyombo ambavyo
vinamamlaka ya kusimamia masuala hayo ya ukatili wa kijinsia viendelea
kusimamia kikamilifu na wale ambao watabainika kuwa wamekuwa na hatia ya
kutenda makosa hayo hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Hatahivyo,amesema ameendelea kutoa elimu
katika shule mbalimbali na mwamko wa upokeaji wa elimu wa masuala ya
unyanyasaji na ukatili wa kijinsia ni mkubwa.
MWISHO
MWISHO
Comments
Post a Comment