Na Mwandishi wetu,Dodoma
SPIKA wa Bunge JOB NDUGAI amesema bunge linatarajia kushauriana
na serikali kuangalia namna ya kuwapima wabunge wote endapo wana maambukizi ya
Virusi vya Ugonjwa wa Corona(COVID 19).
Uamuzi huo unafuatia baada ya ushauri
uliotolewa na mbunge wa jimbo la Kawe HALIMA MDEE aliyeshauri wabunge kupimwa
na kuiomba serikali kutoa taarifa ya hali ya maambukizi ya virusi hivyo ilivyo
nchini kwa sasa.
Akitolea jibu ushauri huo leo bungeni
jijini Dodoma NDUGAI amesema pamoja na kwamba huwenda maabara ya Taifa
itakuwa na foleni ya vipimo vingi lakini watashauriana na wizara husika ili
kuona namna bora ya kulitekeleza hilo na kuwataka wabunge kuwa wamoja katikak
ipindi hiki.
Amewataka wabunge kuchukua tahadhari ya
kukaa umbali wa mita moja baina ya mtu na mtu ili kuchukua tahadhari ya virusi
ikiwa ni namna ya kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalam wa afya.
Pamoja na hilo amewataka wabunge kuendelea
kutoa elimu kwa wananchi wao juu ya namna bora ya kujiepusha na msongamano ili
wajikinge dhidi ya maambukizi ya virusi hivyo.
Comments
Post a Comment