Na.
Bahati Mollel, TAA
WAHASIBU
na Wakaguzi wa Ndani wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wametakiwa
kutumia vyema mafunzo ya uandaaji na uwakilishwaji wa vitabu vya Hesabu za
fedha kwa kuzingatia viwango vya Kimataifa vya Uhasibu kwa Taasisi za serikali
(IPSAS accrual) katika kuboresha ufanisi wao wa kazi wa kila siku, yaliyofungwa
leo kwenye Jengo la Pili la Abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha
Julius Nyerere (JNIA-TB2).
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa TAA, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Uhandisi na
Huduma za Ufundi, Mhandisi Mbila Mdemu alisema amesema kuwa mafunzo hayo yawe
chachu ya kuwabadilisha na kupunguza hoja za ukaguzi.
“Ninaimani
nyote hapa mlishiriki kuanzia siku ya kwanza ya mafunzo haya ya siku tano hadi
mwisho mukiwa na afya njema, hivyo tujitahidi kama wahasibu tusizalishe hoja za
kizembe na tuhakikishe tunasimama kwa miguu yetu kwa kufanya kazi kwa kiwango
na uharaka,” alisisitiza Mhandisi Mdemu.
Amesema
mafunzo haya yamekuja wakati muafaka, ambapo pia yameweza kushirikisha
washiriki kutoka viwanja vyote vilipocho chini ya TAA, ambapo awali kulikuwa na
changamoto chache katika hesabu na kusababisha kuwe na dosari wakati wa
ukaguzi.
“Mafunzo
yatakuwa yamewaongezea ujuzi wa hali ya juu na mtaweza kusaidiana wenyewe kwa
wenyewe maana mmeshiriki wahasibu wa viwanja vyetu vyote pia wakaguzi wetu wa
ndani nao wameshiriki, hivyo kwa njia moja ama nyingine tutakuwa katika nafasi
nzuri ya kupunguza ama kuondoa kabisa hoja za ukaguzi,” amesema.
Pia
aliwashukuru wakufunzi kutoka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Tanzania
(NBAA), kwa kuendesha mafunzo hayo.
Naye
Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Biashara, CPA Josephine Kolola aliishukuru Mamlaka
kwa kukubali kufanyika kwa mafunzo hayo muhimu na ameahidi kuwa watazingatia na
kufanyia kazi vyote walivyo fundishwa.
“Tunaomba
utufikishie salamu zetu kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka na tunaahidi matunda ya
mafunzo haya atayaona kwa Wahasibu wameiva na anaamini hoja za ukaguzi
zitapungua na hata kuondoka kabisa,” amesema CPA Kolola.
MWISHO
Comments
Post a Comment