Na. Mwandishi Wetu, DAR
ES SALAAM
Mkuu wa Jeshi la Kujenga
Taifa (JKT), Brigedia Jenerali Charles Mbuge amesema uwepo wa walinzi SUMA GARD
zaidi ya elfu kumi nchi nzima kumesaidia shirika la SUMA JKT kujiendesha katika
shughuli zake za kiulinzi na hatimaye kupata faida kubwa.
Lengo la kuanzishwa kwa
SUMA JKT ni kusaidia miradi ambayo ina uwezo mkubwa wa uzalishaji ili iweze
kuzalisha zaidi na kwa faida na hivyo kuisaidia Serikali katika kupunguza
matumizi ya kuendesha shughuli za JKT, alisema.
Brigedia Generali Mbuge
ametoa kauli hiyo Jijini Dar Es Salaam katika uzinduzi wa magari manne na
pikipiki tano zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia sita ili
kutekeleza kwa vitendo, nia ya Serikali ya kukuza uchumi wa nchi katika
Viwanda na Biashara kwa maendeleo ya nchi.
Brigedia Jenerali Mbuge
amezitaka taasisi mbali mbali za serikali na binafsi kuwatumia walinzi wa SUMA
GARD ili kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa bodi ya SUMA JKT, Meja Generali mstaafu, Farrah Mohamed amesema
Jeshi hilo lina umuhimu mkubwa katika kujenga malezi kwa vijana hapa nchini,
hatua ambayo itasaidia taifa kupiga hatua katika maendeleo kwa haraka zaidi.
MWISHO
Comments
Post a Comment