Na. Mwandishi Wetu, IRINGA
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mhe.
Richard Kasesela amewataka wanafunzi wa kike kutojirahisisha mpaka kupelekea
kufanyiwa vitendo vya ukatili dhidi yao.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela
akizungumza na wanafunzi wa shule za Sekondari za Wilaya ya Iringa katika Kongamano la wanafunzi la kuupokea msafara wa kijinsia mkoani hapo |
Ameyasema hayo leo mkoani Iringa
wakati akiupokea msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili wa kijinsia
uliposimama mkoani hapo.
Ameongeza kuwa vitendo vya kikatili
vimekuwa vikiongezeka siku hadi siku hasa katika familia na vimekuwa
vikifumbiwa macho na kumalizana kimya kimya.
"Msijirahisishe watoto wangu
mnatupa tabu sana maana tumekuwa tunapambana na vitendo vya ukatili ninyi
mnajirahisisha" alisema.
Mhe. Kasesela amesema kuwa kumekuwa
na ongezeko la mimba na ndoa za utotoni na ulawiti kwa watoto wa kiume watoto
wamekuwa wameharibiwa na kusbabishiwa maumivu na ukatili wa kisaikolojia.
Baadhi ya wanafunzi wa shule za Sekondari Wilaya
ya Iringa wakifuatilia ujumbe wa Msfara wa kijinsia kutokomeza ukatili katika Kongamano la wanafunzi |
Ameongeza kuwa Serikali imejipanga
katika kuhakikisha inasimamia ustawi wa jamii ikiwemo kuwalinda na vitendo vya
kikatili dhidi yao hasa kwa makundi maalum ya wanawake, Watoto na walemavu.
"Tusikae kimya tuseme tutoe
taarifa kwa vyombo vya kisheria kuhusu vitendo vya kikatili vinavyotokea katika
familia na jamii zetu" alisema.
Naye Mwakilishi wa Katibu Mkuu
Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Imelda Kamugisha amesema
vitemdonvyabukatili.vimekuwa vikitokea kwenye jamii zeru na kwa mujibu wa
takwimu wanawake asilimia 30 walio kwenye ndoa wanafanyiwa ukatili wa kijinsia.
"Kutokana na kuongezeka kwa
vitendo vya ukatili Serikali imeongeza vituo vya huduma jumuishi na namba ya
kutoa ripoti ya vitendo vya ukatili kwa watoto ili kuweza kuchukua hatua katika
mapambano dhidi ya vitendo vya kikatili" alisema.
Kwa upande wake Wakili kutoka
Wakala wa Usajili, Ufilisi na udhamini RITA, Janeth Mandawa ametoa wito
kwa wanaume kuandika wosia ili kuondokana na vitendo vya kikatili
vinavyowakumba wanawake wajane katika jamii zetu ili kuwezesha kuwapa haki zao
stahili.
Msanii Nurdin Bilal "Shetta"
akitumbuiza katika Kongamano la wanafunzi Wilayani Iringa la kuupokea msafara wa kijinsia mkoani hapo |
"Sisi tunahusika na
masuala ya wosia kuandika wosia sio kufa ila inasaidia kutoa maelekezo baada ya
mume au mke kufariki ili tuondokane na vitendo vya ukatili"alisema.
MWISHO
Comments
Post a Comment