Na. Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
Katibu Mkuu wa Baraza
la Maaskofu Tanzania (TEC) Padre Dkt. Charles Kitima amesema kipindi cha
kwaresima ni fursa ya kujitafakari na kumpa Mungu nafasi ya kwanza katika
maisha ikiwa ni pamoja na kutambua nafasi ya mwenyezi katika maisha ya kila
siku kwa wakristo na wasio wakristo.
Padre Dkt. Kitima
ametoa kauli hiyo wakati wakristo wakielekea katika mwezi wa toba ambapo
amewataka waumini kote nchini kutambua nafasi ya muumba katika maisha yao
pamoja na kubadilisha mahusiano yao mabaya na Mwenyezi Mungu.
Kwa upande wake, Padre
Hesco Msaga amesema kipindi cha kwaresma ni safari ya kiroho ambayo kila
mkatoliki anatakiwa kutafakari na kujiandaa nafsi yake na kujiweka tayari
katika kipindi hiki cha toba.
Baadhi ya wakristo
wameelezea namna wanavyoutambua umuhimu wa kwaresima.
MWISHO
Comments
Post a Comment