Na. Mwandishi
Wetu, MAKAMBAKO
Mkuu wa
Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri ameagiza kukamatwa kwa walimu mkoani Njombe
watakaobainika kuwafanyia vitendo vya kikatiki wanafunzi ili kukomesha vitendo
hivyo vinavyoendelea kutoka nchini.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Njombe ambaye ni
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe. Ruth Msafiri akiangalia bidhaa za wanawake wajasiriamali alipokuwa akipokea msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili |
Hayo yamebainika
leo Makambako mkoani Njombe wakati msafara wa kijinsia kutokomeza ukatili
ulipofika mkoani humo kwa ajili ya kutoa elimu ya kutokomeza ukatili dhidi ya
wanawake na watoto.
Ruth amesema kuwa
Serikali haipingi adhabu ya viboko ila sio kutoa adhabu ya viboko vya
kupitiliza na kusababisha vilema na maumivu kwa wanafunzi.
Ameongeza kuwa
suala la ukatili ni mapambano makubwa nchini hivyo jitihada zinahitajika kwa
wananchi wadau na mashirika yasiyo ya kiserikali kuhakikisha wanaunganisha
nguvu pamoja kuondokana na vitendo vya ukatili.
Ruth amevitaka
vyombo vya usalama kuacha kufanya ukatili kwa kuchelewesha kesi za vitendo vya
ukatili wa kijinsia na kusababisha ukatili wa kihisia kwa wahanga wa vitendo
hivyo.
Msanii Nurdin Bilal ‘Sheta’ akitumbuiza katika
mji wa Makambako wakati Msafara wa kijinsia uliposimama mkoani Njombe katika kutoa elimu juu ya mapmbano ya vitendo vya ukatili wa kijinsia |
“Vyombo vya
usalama mnachelewesha kesi mnaomba rushwa nawaomba vyombo vys usalama msiwe
kikwazo cha kutopatikana kwa haki ya wahanga wa vitendo vya ukatili” alisema
Ruth.
Akizungumza
kuhusu msaada wa kisheria unaotolewa na Shirika la Legal Serivces Facility,
Joseph Magazi amesema kuwa wameweka nguvu katika kuisidia jamii katika matatizo
ya kisheria kwa kuwawezesha wasaidizi wa kisheria katika mikoa na wilaya kutoa
elimu husika.
"Tumejipanga
kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha tunaifikia jamii katika kutoa elimu
itakayowezesha wenye matatizo mbalimbali ya kisheria kupata msaada na kuyatatua
matatizo yao" alisema Joseph.
MWISHO
Comments
Post a Comment