Na. Jackline Kuwanda, DODOMA
Bima ni sekta ndogo ya fedha yenye umuhimu
mkubwa katika Kujenga uchumi na kuchangia pato la Taifa nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Mamlaka ya
usimamizi wa Bima kanda ya kati (TIRA), Stella Rutahuza wakati akitoa mafunzo
ya uelewa wa Bima kwa waandishi wa Habari jijini Dodoma.
Rutahuza amesema kuwa Bima husaidia kupunguza
makali ya hasara yanayotokana na majanga. Bima pia husaidia kukuza uchumi na
ajira ya kudumu katika Taifa, aliongeza.
Aidha, amesema kuwa Bima zimegawanyika katika
makundi mawili. Alitayaja makundi hayo kuwa ni Bima za mali na ajali, ambapo
kundi hilo ni la muda mfupi na kwa kawaida bima zake humaliza muda wake katika
kipindi kisichozidi miezi 12 haijaendelezwa tena na wahusika katika mkataba.
Wakati huohuo amesema kuwa Bima za mali na ajali
ni kama Bima za vyombo vya moto, meli na mizigo, Ndege, moto. Bima za maisha
amezitaja kuwa ni Bima ya maisha na uwekezaji, maisha na vikundi na Bima ya
vikundi kwa dhamana ya mkopo.
Akizungumzia Bima ya usafirishaji Rutahuza
amesema, Bima hiyo hujumuisha vyombo vya usafiri nchi kavu, reli, ndege, meli, bidhaa
zinazo, dhima ya gari, dhima ya ndege na dhima kwa meli.
Akizungumzia misingi ya Bima na namna ya
kudhibiti majanga Mkurugenzi wa kuendeleza soko la Bima na utafiti wa Mamlaka
ya usimamizi wa Bima Tanzania, Adelaide Muganyizi amesema ilii mkataba wa Bima
ufanye kazi ni lazima uwepo uhusiano unaotambulika kisheria kati ya bima na
kinachowekewa Bima.
Lengo la mafunzo hayo kwa wanahabari ni
kuwajengea uwezo na uelewa ili kuweza kufahamu masuala ya Bima na wao kutoa
elimu kwa jamii ili jamii iweze kutambua faida ya kuwa na Bima katika Maisha
yao ya kila siku.
MWISHO
Comments
Post a Comment