Na. Mwandishi Wetu, DAR
ES SALAAM
Kamati Kuu ya Chama cha
Mapinduzi (CCM) imemvua uanachama Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje, Bernard
Membe.
Hayo yameelezwa leo na
katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole
katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi ndogo za CCM
zilizopo mtaa wa Lumumba hapa jijini Dar es Salaam.
Bernard Membe |
Polepole ameeleza
uamuzi wa kamati kuu ambayo ilitoa siku saba kwa kamati ya nidhamu iliyowahoji
vigogo hao kukamilisha suala lao na kuwasilisha taarifa.
Wakati Membe akivuliwa
uanachama, katibu mkuu wa zamani wa CCM, Abdulrahman Kinana amepewa karipio na
kutakiwa kutogombea nafasi yoyote ndani ya chama hicho kwa miezi 18 huku katibu
mkuu mwingine wa zamani Yusufu Makamba akisamehewa.
Vigogo hao walihojiwa
baada ya sauti zao kusambaa katika mitandao ya kijamii wakieleza jinsi CCM
inavyopoteza mvuto na jinsi chama kilivyoshindwa kuwalinda makatibu hao dhidi
ya mtu anayejiita mwanaharakati, ambaye alikuwa akitoa tuhuma dhidi yao.
MWISHO
Comments
Post a Comment