ACT WAZALENDO KUSIMAMIA UADILIFU NA DEMOKRASIA UCHAGUZI WA NDANI


Na. Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya Taifa ya chama cha ACT Wazalendo, Omari Shaban amesema chama hicho kimejipanga kusimamia uadilifu na demokrasia katika uchaguzi wa ndani wa kuwapata viongozi wa kitaifa wa chama hicho na kuhakikisha uchaguzi huo unafuata misingi ya katiba na sheria za uchaguzi.

Mwenyekiti wa kamati hiyo ya uchaguzi ndani ya ACT Wazalendo ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho kijitonyama jijini Dar es salam wakati akitoa taarifa ya zoezi la uchukuaji na urejeshaji fomu za wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi wa chama hicho.

Akifafanua kuhusu tuhuma za baadhi ya wagombea wa chama hicho kushinikizwa kubadilisha nafasi za kugombea uongozi Shaban amekanusha tuhuma hizo na kueleza kuwa kamati hiyo imekuwa ikiwahamasisha wanachama kuwania uongozi na sio kuwashinikiza kubadili nafasi za kugombea.

Vikao vya uteuzi wa wagombea wa nafasi za uongozi ndani ya ACT Wazalendo unatarajiwa kuanza Machi mosi mwaka huu.

MWISHO

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.