YALIYOJIRI WAKATI WA KIPINDI CHA TUNATEKELEZA KILICHOMSHIRIKISHA MKUU WA MKOA WA NJOMBE, CHRISTOPHER OLE SENDEKA JANUARI 30, 2020
# Bilioni zaidi ya
500 zimetolewa na Serikali katika ujenzi wa miundombinu ya barabara kwa
kiwango cha lami kuunganisha Wilaya zote na makao makuu ya mkoa
#Serikali ya Awamu
ya Tano imetimiza matarajio ya wananchi wa mkoa wa Njombe kupitia ujenzi wa
miundombinu ya barabara, vituo vya afya, maji na elimu
#Mkoa wa
Njombe uko salama hali inayowezesha wananchi kutekeleza shughuli za
uzalishaji na kujiletea maendeleo
#Ujenzi wa
miundombinu ya barabara unawezesha utekelezaji wa miradi ya kimkakati kama ule
wa Chuma cha Liganga na Mchuchuma kwa maslahi ya Taifa
#Jengo la wagonjwa
wa nje (OPD)limekamilka na kuanza kutoa huduma kwa wananchi
#Bilioni 4.5
zilitolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali za Wilaya
#Vituo 7 vya afya
vimepatiwa fedha za upanuzi katika mkoa wa Njombe
# Mkoa wa Njombe
umefanikiwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo
# Ujenzi wa
miundombinu utawezesha kukua kwa biashara katika mkoa wa Njombe
# Tumejenga kiwanda
kipya cha kusindika chai katika mkoa wetu na pia tumejenga viwanda vya kati na
vidogo
#Tumepata kiwanda
cha kuzalisha mafuta yanayotokana na zao la parachichi
# Kiwanda cha
kufungasha maparachichi na kusafisha nje ya nchi nacho kinafanya kazi
vizuri
# Mwitikio wa
wananchi kuzalisha zao la parachichi ni mzuri na mkoa umeweka utaratibu wa
kuwafuatilia na kuwasaidia
# Mkoa wa Njombe
unanufaika na mradi wa gridi ya Taifa kutoka kituo cha kupoza umeme Makambako
hivyo kuna umeme wakutosha
# Mkoa wa Njombe
una maeneo mazuri ya uwekezaji, hivyo tunawakaribisha wawekezaji wa ndani na
nje
Imeandaliwa na
Idara ya Habari MAELEZO
Comments
Post a Comment