Na. Mwandishi Wetu,
DODOMA
WAZIRI Mkuu Kassim
Majaliwa amesema kama msimamizi wa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama
Cha Mapinduzi (CCM) ataendelea kulinda wawekezaji wa ndani na atakuwa mkali
pale anapoona kuna mambo hayaendi sawa.
Majaliwa ametoa
msimamo huo leo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la papo kwa papo la
Mbunge Jaku Ayoub aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itafikiria Sukari inayozalishwa
katika kiwanda cha Mahonda Zanzibar angalau kidogo ikaja kuuzwa Tanzania Bara
kama ilivyo kwa bidhaa nyingine zinazozalishwa Tanzania Bara kuuzwa Zanzibar.
Akijibu swali
hilo Waziri Mkuu amesema alipofanya ziara alikuta sukari nyingi ipo bohari
imejaa na kwamba kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha tani elfu 24,000 lakini
hivi sasa kinazalisha tani 6,000.
MWISHO
Comments
Post a Comment