WASICHANA WENYE UMRI WA MIAKA 10 – 25 JIJINI DODOMA KUPATA ELIMU JUU YA LISHE BORA

Na Mwandishi wetu, Dodoma

Taasisi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Girl Guide Association imezindua mpango wa kuhamasisha Lishe kwa vijana wa kike wenye umri wa kuanzia miaka Kumi mpaka 25 Jijini Dodoma, baada ya tafiti kuonesha kuwa vijana wa umri huo wamekua katika hatari ya kutokua na Lishe bora pamoja na upungufu wa Damu. 


Yusta Kobelo 

Akizungumza mbele ya kikao cha balaza la Madiwani Jijini Dodoma, baada ya kupata kibali kwa mujibu wa sheria na taratibu za Balaza hilo Kiongozi wa Utetezi Lishe wa taasisi hiyo Yusta Kobelo amesema kazi yao kubwa ni kutembelea katika shule za Msingi, Sekondari pamoja na vyuo ili kutoa Elimu ya jinsi gani vijana hao wanaweza kuboresha Afya katika mazingira yao ikiwa ni pamoja na aina ya vyakula, mboga pamoja na matunda.

Kobelo alisema kuwa ndani ya mpango huo wana kampeni inayoitwa Sahani ya Upinde wa Mvua (rainbow plate) ambayo lengo kubwa ni kuhakikisha kwenye kila sahani anayoishika mtoto wa kike kwaajili ya chakula iwe na Protini, Vitamini pamoja na Wanga hata kwa uchache ili kutengeneza jamii yenye Afya iliyoimarika.

“Imeonekana Wasichana wa sasahivi wanapenda kuwa na mwili mdogo, wanapenda diet lakini hawajui nini wale nini waache, utakuta msichana anatumia chips kidogo au keki na soda alafu usiku hali kabisa, tunajaribu kuwashawishi kwamba kula ugali na dagaa kwa kiasi kidogo unaweza uka maintain afya yako, kwa sababu katika vyakula kama hivi kuna virutubisho ambayo vikizidi vinaleta uzito uliozidi na vikipungua vianaleta utapiamlo, kwaiyo tunatamani wasichana wajifunze mengi kuhusiana na lishe bora” Aliongeza Kobelo.

Akizungumzia changamoto walizonazo alisema kubwa ni taizo la kutokua na ofisi Jijini hapa hivyo alimuomba Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kuwasaidia kutatuza changamoto hiyo ambapo ikitatuliwa itawasaidia wao kupata nafasi ya kuzungumza na wasichana katika hali ya usiri kwani wapo wenye matatizo ambayo hawawezi kuyazungumza hadharani lakini wakiwa na ofisi itawasaidia kuwa karibu nao zaidi.

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.