Na.
Dennis Gondwe, DODOMA
WAFANYABIASHARA
katika masoko ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma wametakiwa kufanya biashara zao
katika maeneo rasmi waliyotengewa ili kutokwamisha shughuli nyingine za kijamii
kuendelea.
Afisa Masoko, James Yuna |
Kauli
hiyo ilitolewa na afisa masoko wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, James Yuna
alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha Dodoma ‘Live’ kinachorushwa na kituo cha
redio cha Dodoma FM.
Yuna
alisema kuwa imezuka tabia kwa baadhi ya wafanyabiashara kupanga biashara zao
nje ya maeneo waliyopangiwa katika masoko jijini hapo. “Upangaji wa biashara
nje ya masoko ni kinyume na utaratibu. Wapo baadhi ya wafanyabiashara
wanaopanga bidhaa zao nje ya masoko na wengine barabarani. Utaratibu huu
unazuia huduma nyingine kuendelea katika Halmashauri ya Jiji. Barabarani ni
sehemu ya kupita magari na waenda kwa miguu” alisema Yuna.
Kufanyia
biashara maeneo hayo tunahatarisha maisha ya wafanyabiashara hao pindi ajali
inapotokea, aliongeza. Aidha, kuwa kufanya biashara maeneo yasiyo rasmi
kunahatarisha usalama wa bidhaa zinazouzwa ikiwa ni pamoja na usafi.
Afisa
Masoko huyo aliwataka wafanyabiashara katika masoko ya jiji hilo kufanya
biashara kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa.
MWISHO
Comments
Post a Comment