Na. Mwandishi Wetu,
DODOMA
SERIKALI imewasihi
wazazi wenye watoto wanaosoma nchini China waliorudi kwa ajili ya likizo
kutowaruhusu kurudi mpaka hapo watakapopata mawasiliano ya kidiplomasia kuhusu
maendeleo ya mlipuko wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na
kirusi aina ya ‘Corona’.
Tahadhari
hiyo ameitoa jana bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la papo kwa papo
la Mbunge wa Mafinga Mjini, COSATO Chumi aliyetaka kujua serikali imejipangaje
kukabiliana na kudhibiti virusi vya ugonjwa huo ambao kwa namna moja ama
nyingine unaathiri ukuaji wa maendeleo wa Taifa na wananchi kwa kukizingatia
kuna biashara kubwa kati ya Tanzania na China.
Waziri
Mkuu amekiri kuwa ni kweli kwamba China kuna ugonjwa wa virusi ya ‘Corona’
unaopoteza maisha ya watu na sasa wameanza kuona nchi za jirani yake wameanza
kupata maambukizi hayo.
Amewahakikishia
kuwa Tanzania haina ugonjwa huo wa ‘Corona’ na jana Waziri wa Afya na Naibu Waziri
wa Afya wametoa taarifa za ugonjwa huu.
MWISHO
Comments
Post a Comment