SERIKALI KUJENGA DAMPO DAR ES SALAAM


Na. Mwandishi Wetu, DODOMA
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mussa Zungu amekiri kuwa ni kweli hali ya uchafu katika Jiji la Dar es Salaam ni kubwa kutokana na uwepo wa dampo moja na kuahidi kujengwa dampo jipya la kisasa litakalobeba taka zote.
Hayo ameyasema jana bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kawe, Halima Mdee aliyetaka kujua mpango wa serikali wa kujenga dampo la kisasa kwenye maeneo mengine kila wilaya ili kuzuia uchafu kutokana na lililopo kutokidhi kubeba uchafu katika jiji zima.
Akijibu swali hilo Zungu amesema kasi ya taka katika Jiji la Dar es Salaam ni kubwa licha ya kuwa linakua kwa kasi na kwamba miaka ijayo linakadiriwa kuwa na watu zaidi ya milioni 8 hadi 9 na dampo ni moja.

MWISHO

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.