Na. Jackline
Kuwanda, DODOMA
Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha na Mipango, Mary Maganga amelihimiza baraza la wafanyakazi la
Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya rushwa.
Pia amelitaka baraza
Hilo kufanya kazi kwa kuzingatia uwajibikaji na misingi
ya Maadili kwani ni nguzo muhimu kwa maendeleo ya Taifa.
Akizungumza Jijini Dodoma
wakati akifungua mkutano wa kwanza wa baraza la
wafanyakazi wa ofisi ya Taifa ya Ukaguzi 2019/2020, amesema ni
muhimu kwa baraza hilo kufanya kazi kwa maadili na nidhamu ya hali
ya juu kwani ni jicho la watanzania katika masuala ya ukaguzi wa rasilimali
za umma.
Kwa upande wake Mdhibiti na Mkaguzi
mkuu wa hesabu za serikali (CAG), Charles Kichere ambaye pia ni mwenyekiti wa
baraza la wafanyakazi Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi amesema lengo kuu la mkutano
huo ni kupitia na kuidhinisha makadilio ya bajeti ya ofisi ya Taifa ya ukaguzi
kwa mwaka wa fedha 2020/2021 kama inavyoelekezwa kwenye waraka Na.1
wa mwaka 1970.
Katika hatua nyingine Kichere
amesema kuwa baadhi ya changamoto zinazoikabili ofisi hiyo ni
pamoja na uhaba wa fedha unaokwamisha majukumu ya ofisi ,mgao wa fedha kutokuja
kwa wakati na usiotosheleza mahitaji, mishahara midogo kwa wafanyakazi.
Naye, Jenijely James, Katibu wa
kamati za Wanawake -TUGHE Taifa amesema baraza hilo ni nguzo muhimu
kwa maendeleo huku Tumainiel Mshomba ambaye ni ambaye ni katibu wa
baraza la wafanyakazi ofisi ya Taifa ya Ukaguzi akisema muundo wa baraza hilo
lina wajumbe 110.
MWISHO
Comments
Post a Comment