Na. Mwandishi Wetu,
DODOMA
ALIYEKUWA Waziri wa Mambo
ya ndani ya Nchi, Kangi Lugola leo amefika Makao Makuu ya Ofisi za Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuhojiwa.
Kangi amehojiwa takribani
saa6 Katika Ofisi jizo zilizopo eneo la Jamhuri jijini Dodoma kuanzia majira
moja na dakika24 asubuhi kwa ajili ya kuhojiwa ambapo alitoka saa6na dakika35.
Kangi ambaye kwa sasa ni
Mbunge wa Mwibara (CCM) na wenzake watatu ambao ni aliyekuwa Kamishna Jeneral
wa Zimamoto na uokoaji, Thobias Andengenye, Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Jacob Kingu na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi
Hamad Yusuph Masauni wote watahojiwa leo kwa nyakati tofauti.
Wote wanne wanahojiwa
kufuatia agizo la Rais, Dk.John Magufuli kufuatia mkataba ilioingiwa na wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi wa Sh.trilioni 1.
Mwisho
Comments
Post a Comment