Na.
Dennis Gondwe, DODOMA
HALMASHAURI
ya Jiji la Dodoma inajivunia kutoa fursa kwa wafanyabiashara kuweza kufanya
shughuli zao katika masoko yake na kukuza kipato chao na taifa kwa ujumla.
![]() |
Afisa Masoko, James Yuna |
Kauli
hiyo ilitolewa na afisa masoko wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, James Yuna alipokuwa
akiongea katika kipindi cha Dodoma ‘Live’ kinachorushwa na kituo cha redio cha
Dodoma FM.
Yuna
alisema kuwa Halmashauri inajivunia fursa inayotoa kwa wafanyabiashara kuweza
kufanya shughuli zao katika maeneo ya masoko yaliyopangwa kwa mujibu wa
taratibu. “Ndugu mtangazaji, mafanikio ni mengi katika eneo hili la masoko.
Tumeweza kusajili idadi kubwa ya wafanyabiashara katika masoko yanayomilikiwa
na Halmashauri ya Jiji. Kikubwa zaidi ni ukusanyaji mapato katika masoko hayo”
alisema Yuna.
Halmashauri
ya Jiji inaendeshwa kwa mapato yanayokusanywa kutoka katika vyanzo mbalimbali,
hivyo masoko ni sehemu muhimu ya kuwezesha upatikanaji wa mapato hayo,
aliongeza.
Afisa
masoko huyo aliwataka wafanyabiashara hao kulipa mapato kwa mujibu wa sheria.
Huduma zote zinazotolewa katika Halmashauri zinahitaji fedha ili zitekelezwe,
aliongeza.
MWISHO
Comments
Post a Comment