JESHI LA POLISI LAUA 5 WANAOSADIKIWA MAJAMBAZI


Na. Mwandishi Wetu, ARUSHA
Polisi Mkoa wa Arusha wamewauwa watu watano wanaosadikiwa kuwa majambazi  katika eneo la Matevez Kata ya Olmot jijini Arusha ambapo yalitokea  majibizano ya risasi kati ya washukiwa hao na Jeshi la Polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna msaidizi wa Polisi, Jonathani  Shana akiongea na waandishi wa habari, amesema watu hao wananodaiwa kuwa ni majambazi walikuwa safarini kuelekea wilayani Simanjiro mkoani Manyara kwenda kufanya tukio la ujambazi na ndipo jeshi hilo lilipopata taarifa kutoka kwa raia wema.

Katika hatua nyingine kamanda Shama ametaja baadhi ya vitu vilivyopatikana vinazodaiwa kuibiwa katika eneo la Olasiti ikiwemo bunduki moja aina ya Shortgun na simu mbili ambazo tayari zimetambuliwa kuwa ni mali ya Jackson Msangi.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Arusha ambae pia ni Mkuu wa Mkoa huo, Mrisho Gambo ameleezea tukio hilo kama salama za mkoa kwa waziri mpya wa mambo ya ndani George Simbachawene.

Jackson Msangi na Nikira Msangi ni baadhi ya wahanga wa tukio la ujambazi ambao wanalipongeza jeshi hilo kwa kufanikisha upatikanaji wa baadhi ya mali zilizoibiwa na watu hao.
Baada ya dakika thelethini na tano za majizano ya risasi kazi imebaki kwa wananchi kutambua miili ya watu hao iliyohifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Mount Meru.

MWISHO 

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.