Na.
Gibson Gabriel,
Klabu
ya Yanga imeibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons ya Mbeya
katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara uliochezewa katika uwanja wa kumbukumbu
ya Samora mkoani Iringa.
![]() |
| Picha kwa hisani ya mtandano |
Mechi
hiyo ilichezwa katika uwanja wa Samora kutokana na uwanja wa Tanzania Prisons
kufungiwa baada ya kuharibiwa na Bodi ya ligi kuchukuwa maamuzi ya kuhamishia mchezo
huo mjini Iringa.
Katika
mchezo huo, Yanga walijipatia goli hilo la ushindi mapema baada ya kiungo
mshambuliaji Patirick Sibomana kutumbukiza nyavuni mpira ulirushwa na Abdalah Azzi
Makame.
katika
mchezo huo Yanga walicheza kwa kuelewana ambapo walimudu kulidhibiti eneo hilo
la kiungo na kufanya Tanzania Prisons kuzidiwa katika safu hiyo ya kiungo.
kocha
wa Yanga, Charles Mkwasa amepongeza
kikosi chake kwa kucheza vizuri licha ya mchezaji wake, Deus Kaseke kupata
majeruhi katika mchezo huo ambao ulikuwa mzuri na wakuvutia.
Kwa
upande wake kocha wa Tanzania Prisons, Adolf Richard amekili kupoteza mchezo huo licha ya
kuwasifu wachezaji wake kucheza kwa
kujituma.
Nao
baadhi ya mashabiki wa Yanga mkoani Tabora, Mohamed Bakar na Shija Lusana
wamesema "tumefurahishwa na timu yetu kwa kucheza vizuri kwa hali hii
tunaenda kuchukua pointi tatu mbele ya Simba tarehe 4 Januari, 2020" alisema
Bakar.
Yanga
ikiwa na michezo kumi iliyocheza ligi kuu tayari imejikusanyia pointi 21
ikishika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo.
=30=

Comments
Post a Comment