Na.
Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
Wabunifu nchini wametakiwa kuhakikisha wanazisajiri bunifu zao
ili kuweza kuzilinda na kujipatia manufaa katika bunifu hizo na hatimaye
kukuza uchumi wa nchi na maendeleo ya jamii kwa ujumla.
Rai hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na afisa mtafiti
kutoka kituo cha uhawilishaji wa teknolojia ambaye pia ni mtaalamu wa masuala
ya haki miliki na bunifu kutoka COSTECH, Judith Kadege ambapo amesema
kuwa Kufuatia kuwepo kwa changamoto hiyo ya kutosajiri bunifu hizo Tume
ya Sayansi nchini ikaamua kuja na semina ya siku nne ya kuwajengea uwezo
wabunifu wa mashindano ya kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU)
ili kuweza kuwasaidia wabunifu hao namna ya kulinda bunifu zao na kujua
nyezo ambazo wanaweza kuzitumia.
Aidha, amesema kuwa kuwakutanisha wabunifu hao kutaweza
kuwasaidia kujua wapi wapeleke bunifu zao ili kuweza kufanyika kazi na
pia kuwawezesha wamiliki uwezo wa kuongea na makumpuni makubwa
kuweza kutumia teknojia za wabunifu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kitengo cha
uhawilishaji wa kiteknolojia Dkt. Athumani Mgumi amesema kuwa lengo
la mafunzo hayo ni sehemu ya ahadi ya serikali katika kuendeleza bunifu ili
kuboresha teknolojia zao.
Semina ya siku nne ya kuwajengea uwezo wabunifu wa
mashindano ya kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) inatarajiwa
kufungwa na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
=30=
Comments
Post a Comment