Na.Gibson
Gabriel, TABORA
Msimamizi
wa kituo cha mradi wa kilimo cha umwangiliaji katka eneo la Maili tano kilichopo
Kata ya Ipuli mkoani Tabora Said Omary amewataka vijana kujiendeleza katika
kilimo cha bustani ili kujikwamua kiuchumi.
![]() |
Bustani ya Nyanya |
Akiwa
katika sehemu ya kazi, Omary amesema kuwa kilimo cha nyanya kinaweza kukuza
kipato cha mtu bila kutengemea ajira kutoka serikalini. "Mfano kama aina
ya Segefu one ambayo ni aina ya nyanya ambayo inakuwa kwa kupanda juu ambapo
ukianza kuvuna uchukuwa miezi mitatu ukilinganisha na aina nyingine” amesema Omary.
Kwa
upande mwingine Omary amefafanua kuwa aina hiyo ya nyanya hudumu kwa muda mrefu
hivyo husaidia kupata faida kutokana na kutoa matunda mengi kwa muda mrefu.
Aidha,
kilimo cha bustani ya nyanya kimekuwa kikisaidia kuinua kipato kutokana na
kilimo hicho kuwa na bei kubwa hasa pale shamba likianza kuivisha matunda.
Kutokana
na kilimo cha bustani ya nyanya kimemsaidia Omary kununua kiwanja. Aidha, amewataka
vijana kutopuuzia kilimo hicho kwa sababu husaidia kubadilisha hali ya
kimaisha.
Nae
Martine Anthony anayefanya biashara ya nyanya amesema kilimo cha nyanya
anakipenda kwa sababu humwingizia kipato kikubwa kinachomfanya kumundu mahitaji yake ya kimaisha.
vijana
wengi wamekuwa wakikataa kufanya kazi wakisubilia ajira ambazo ni ngumu katika
wakati huu na kuwashauri kuodoa woga wa kuthubutu kuanzisha vitu ambavyo vitawainua
kuuchumi.
Comments
Post a Comment