Na.
Mwandishi Wetu, SINGIDA
Ofisi ya Wakala wa Barabara za Vijijini
na Mijini (TARURA) Wilaya ya Singida imesema itaendelea Kutoza faini kwa madereva
wanawaokiuka sheria za maegesho ili kufanikisha mpango wa Serikali juu kukusanya
mapato Kupitia ushuru wa maegesho yaliyo rasmi.
Akizungumza na Mtandao wa Dodoma News Ofisini
kwake, Meneja wa TARURA Wilaya ya Singida, Injinia Elgidius Method amekiri kuwa
zoezi la utozaji faini kwa madereva lipo na ni endelevu lengo likiwa ni kudhiti
uegeshaji usio rasmi unaopelekea Serikali kupoteza mapato ya ushuru wa maegesho.
Amesema TARURA wamepewa dhamana ya kuchukua
ushuru wa maegesho katika kaeneo ya maegesho. Alisisitiza kuwa utaratibu huo
unafanyika pia katika Mikoa mingine ili Kuepusha madhara yanayoweza kusababishwa
na uengeshaji kiholela na kurahisisha kukusanyaji wa ushuru.
Kauli ya Meneja wa TARURA Wilaya ya
Singida inakuja siku chache baada ya kikao baina ya Mkuu wa Kitengo cha Usalama
Barabarani Mkoani Singida na madereva wa Bajaji na Bodaboda kilichoibua sintofahamu
kuhusu TARURA namna wanavyotoza faini kwa madereva.
Mmoja wa madereva wa Bajaji mkoani
Singida, Hassan Mapunda ambaye alihudhuria katika kikao hicho amesema TARURA wameenda
mbali zaidi katika wajibu wao ambapo wamekuwa wakiwakamata pasipo sababu ya msingi.
Mapunda amesema TARURA wanapaswa
kukutana na madereva na kuwapa maekelezo juu ya namna wanavyotakiwa kufanya badala
ya kuwatoza faini bila ya kuwapa utaratibu maalumu wa kufuata.
=30=
Comments
Post a Comment