Na. Edith Shija
Rais Dkt. John
Magufuli jana tarehe 27 Disemba, 2019 alifanya usajili wa laini yake ya simu ya
mkononi kwa alama za vidole na kuwataka watanzania wote wanaotumia simu
kusajili laini zao kwa alama za vidole kama ilivyoelekezwa na Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA), alitangaza kuongeza siku 20 kwa ambao hawajakamilisha
zoezi hilo kukamilisha.
Rais Dkt. Magufuli
alifanya usajili huo wa laini yake mjini Chato mkoani Geita ambapo aliongeza
siku 20 kuanzia Januari 01, 2020 hadi Januari 20, 2020 kwa wote ambao
watashindwa kusajili laini zao Katika kipindi cha kuishia tarehe 31 Disemba,
2019.
Aidha, Rais alisisitiza
baada ya siku hizo 20 alizoongeza kukamilika hakutakuwa na kisingizio chochote
kile kitakachokubalika na aliiagiza TCRA kuhakikisha laini ambazo
hazijasajiliwa zinazimwa baada ya tarehe hiyo.
Hata hivyo Rais
Magufuli amefafanua kuwa usajili wa Laini za simu kwa alama za vidole ni muhimu
kwa usalama wa nchi ikiwemo kuepusha vitendo vya utapeli na ujambazi
vinavyofanywa na wahalifu ambao wengi wao hukamatwa na vyombo vya dola.
=30=

Comments
Post a Comment