Na.
Gibson Gabriel
Klabu
ya soka ya KMC ya Dar es Salaam imekubali kipigo cha magoli 2-0 kutoka kwa
mabingwa watetezi Tanzania bara Simba SC katika mchezo uliopingwa katika uwanja
wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
![]() |
Wachezaji wa Simba wakishangilia goli |
Katika
mchezo huo Simba walianza kujipatia goli la kwanza kupitia kwa Deo Kanda baada
ya kupokea pasi murwa kutoka kwa Hasani Dirunga na kuiandikia Simba goli la
kwanza.
KMC
ikiwatumia viungo Kenny Ally, Batista Mgiraneza, Boniface Magaga walionekana
wakijitahidi kuimudu Simba mnamo kipindi cha kwanza kitu kilichomfanya kocha wa
Simba kuwatumia mawinga kuishambulia KMC kutokea pembeni.
Katika
mchezo huo magoli yote ya Simba yalipatikaa kipindi cha pili kupitia kwa Deo
Kanda na Gerson Fraga aliye funga goli hilo nje ya eneo la 18 katika dakika za
nyongeza.
Baada
ya mchezo wa KMC kupoteza imebaki katika nafasi ya 17 katika msimamo wa ligi
kuu Tanzania bara ikiwa katika hatari ya kuchezea mstari wa kushuka daraja kama
wataendelea kupoteza michezo.
Kuingia
kwa viungo Clotus Chama na Fras Kahata kulibadilisha sura ya mchezo ambapo waliongeza presha kwa KMC
wakajikuta wakifungwa goli hizo 2-0.
Kutokana
na mchezo huo KMC wamebaki nafasi ya 17 na point 9 huku wakimfanya Simba SC
kuendelea kujikita kileleni akiwa na pointi 31 na michezo 12 aliyocheza ya ligi
kuu Tanzania bara msimu huu.
Ikumbukwe
klabu ya KMC msimu jana walimaliza katika nafasi ya nne ambayo iliwapeleka
kucheza michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.
Comments
Post a Comment