Na.
Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
Serikali
ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania imepokea msaada wa fedha wa zaidi ya
shilingi bilioni nne kutoka kwa serikali ya Japan kwa ajili ya kufufua shirika
la Uvuvi Nchini –TAFICO wenye lengo la kuboresha maisha ya wananchi kiuchumi.
Kupitia
msaada huo vifaa mbalimbali vitanunuliwa ikiwa ni pamoja na meli ya Uvuvi yenye
vifaa vya kisasa, mashine ya kutengeneza barafu, ghala la baridi la kuhifadhi
samaki pamoja na gari la lenye mitambo maalumu ya barafu na gari aina ya ‘Pickup’
kwa ajili ya kusambaza samaki.
Akizungumza
katika utiliaji saini juu ya mkataba huo Jijini Dar es Salaam, Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James amesema mradi huo
utaongeza uuzaji wa samaki nje ya nchi ambapo kiwango cha ukuaji kwa
shughuli ndogo zilifikia zaidi ya asilimia 9 pamoja na kuchangia pato la Taifa
kwa asilimia 1.7 kwa mwaka 2018.
Naye
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Rashid Tamatamah ameeleza kuwa
mradi huo utaisaidia sekta hiyo kufanya kazi kisasa kutokana na kununuliwa kwa
vifaa mbalimbali ambapo mchakato huo ulianza tangu Januari 2018.
Kwa
upande wake mkuu wa ushirikiano wa maendeleo, Ubalozi wa Japan, Shintaro
Hayashi amesema Serikali ya Japan imekuwa ikiisaidia Serikali ya
Tanzania ambapo licha ya mkataba huo Serikali ya Japan imesaidia katika
maeneo mengine ikiwa ni pamoja na miundominu kama vile barabara, sekta ya
Maji, sekta ya Kilimo pamoja na Afya.
=30=
Comments
Post a Comment