Na. Mwandishi Wetu, CHAMWINO
Taasisi zinazotete haki
za watoto zimeombwa kutembelea maeneo ya vijijini ili kuhamasisha umuhimu wa
elimu kwa wanafunzi hususani watoto wa kike.
Hatua hiyo imekuja
kufuatia baadhi ya wazazi na walezi kuwaeleza watoto wao kufanya vibaya katika
mitihani ya kuhitimu darasa la saba ili waweze kuwaozesha na kujipatia kipato.
Jenifa Mwombeki ni
mwalimu katika shule ya msingi Nzali iliyopo wilayani Chamwino amesema
wanafunzi wanahitaji kushauriwa vizuri ili kuachana ushauri wa kuwataka kufanya
vibaya kwa makusudi.
Joyce ni binti mwenye
ulemavu wa ngozi ni miongoni mwa wanafunzi waliomaliza darasa la saba katika
shule ya msingi Nzali anasema haikuwa rahisi kumaliza kwa sababu alipitia
vishawishi hivyo vya kuelezwa kufanya vibaya kwa makusudi katika mitihani ya
darasa la saba.
“Nilipofika darasa la
saba vilikuja vishawishi ambavyo vilikuwa vinanitisha vingine na kunifanya
viongope. Lakini mimi sikusikiliza hizo sauti, wazazi wangu pamoja na wengine
walikuwa wananiambia nijifelishe maana nitachaguliwa shule ya mbali. Lakini mimi
sikusikia hizo sauti nikafanya vizuri matokeo yalipotoka nikawa nimepangiwa Tumaini
sekondari ambayo ipo singida shule ya wasichana. Fomu ilipokuja ilikuwa na
mahitaji mengi na laki nane ukiangalia na uchumi wa nyumbani ikawa
inashindikana” anasema Joyce.
Aidha, aliwashauri wazazi kuwaacha watoto wasome
ili watimize ndoto zao.
Mtandao wa Dodoma
News umezungumza na baadhi ya wazazi ambapo wamesema ili kuondokana na
tatizo hizo ni lazima kuwepo kwa ushirikiano kati ya wanafunzi, walimu na
wazazi.
=30=
Comments
Post a Comment