Faru Fausta Afariki Dunia Akiwa Na Miaka 57


Na. Mwandishi Wetu,

Faru Fausta ambaye alikuwa akiaminika kuwa ndiye Faru Mzee zaidi Duniani amefariki akiwa na umri wa miaka 57 hapa Nchini, Faru huyo ameishi maisha yake yote Katika hifadhi ya Ngorongoro mpaka umauti ulipomkuta jana Disemba 27, 2019.
 
Faru Fausta
Mhifadhi mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCA) Dkt. Fredy Manongi amesema Fausta ndiye alikuwa Faru mzee zaidi Duniani. 

"Tunahisi kifo chake ni cha kawaida kutokana na umri wake kuwa mkubwa madaktari wapo njiani watatuelezea hasa sababu ya kifo chake baada ya kufanya vipimo" ameeleza Dkt. Manongi

Aidha, Faru huyo jike alikuwa chini ya uangalizi maalumu kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita baada ya afya yake kudhoofika na kuanza kushambuliwa na wanyama wakali mwituni.

"Wanyama wakali hususani Fisi walianza kumshambulia na akapata vidonda vikubwa sana lakini ilipofika mwaka 2016 ilibidi tumtoe porini na kumuweka kwenye uangalizi maalumu vidonda vyake vilipona lakini afya yake bado ilikuwa dhoofu hatukuweza kumrejesha porini" amesema Dkt. Manongi. 

Faru Fausta licha ya umri wake kuwa mkubwa hakuwahi kuzaa na hiyo inaelezwa huenda ikawa ni moja ya sababu ya kuishi kwake kwa muda mrefu.

Hata hivyo Faru wanakadiriwa kuweza kufikisha umri wa miaka 37 hadi 43 wakiwa porini na huweza kufikisha hadi miaka 50 wakifugwa katika maeneo maalumu, pia Faru mweusi mwingine wa mwituni ambaye alifahamika kwa umri wake mkubwa ni Solio jike lililokuwa likiishi Kenya na kufariki likiwa na miaka 42 mwaka 2016.
=30=

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.