Na.
Mwandishi Wetu, DODOMA
Wananchi wa Mtaa wa Hazina Jijini Dodoma waelezea changamoto
wanazokumbana nazo katika kivuko cha miguu katika kipindi cha mvua.
Wakizungumza na Mtandao wa Dodoma News wamesema
kuwa wanakutana na changamoto za kupita katika eneo hilo ikiwa ni udogo wa
kivuko hicho pamoja na ubora wake ukilinganisha na idadi ya watu wanaopita
hapo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Hazina, Azizi Seif
amesema kuwa tatizo la kivuko limekuwa changamoto na pia hakikidhi mahitaji ya
watumiaji wa mtaa huo kutokana na udogo wa kivuko hicho na
kiwango kilichojengwa ukilinganisha na pesa zilizotumika.
Aidha, ameongeza kuwa mazingira ya eneo hilo ni hatarishi
hasa kwa watoto kuchezea Maji machafu na kwa walemavu kupata ugumu
wa kuvuka kutoka mtaa mmoja kwenda mtaa wa pili kutafuta huduma za
kijamii.
Ikumbukwe kuwa katika kipindi cha nyuma kilichopita eneo
hilo lilisababisha maafa kwa Maji kumsomba mtu mmoja na mifungo mbalimbali
hivyo wananchi wanaoishi pembezoni mwa eneo hilo wametakiwa kuwalinda
watoto wao wasichezee Maji machafu ili kuwakinga dhidi ya magonjwa ya mlipuko.
=30=
Comments
Post a Comment