Na. Jackline Kuwanda, DODOMA
Afisa Mtendaji wa kijiji cha Mpwayungu wilayani Chamwino mkoani Dodoma, Seleman Kibakaya amesema kuwa katika kijiji hicho wameunda mabaraza ya watoto katika ngazi ya kata na kijiji ili kuibua haki za watoto pamoja na kupinga vitendo vya kikatili dhidi ya watoto.
Akizungumza na Dodoma news kijijini hapo, Kibakaya amesema mabaraza hayo ni muhimu kwa watoto kwani wanapoona vitendo vya kikatili vimetokea katika maeneo yao moja kwa moja huenda katika mabaraza hayo kutoa taarifa za vitendo hivyo na hatua huchukuliwa.
Katika hatua nyingine kibakaya amesema katika kijiji hicho kumekuwa na changamoto kwani baada ya kuwa washughulikia kesi ya unyanyasaji wa mtoto ikiwemo mwanafunzi kupewa mimba baadhi ya wazazi huchukua hatua ya kuwatorosha hao hali inayoleta ugumu katika kesi hizo kwa kukosa ushahidi.
Amesema kikubwa wanachokifanya kwa upande wa wanafunzi wa kike wamefanya jitihada kubwa na walimu za kuwafanyia uchunguzi wanafunzi wote wa kike kila mwezi kama wakibaini mwanafunzi ameshika ujauztio hatua huchuliwa .
Mbali na hilo amesema kinachosababisha wazazi katika kijiji hicho kuwaozesha watoto wa kike katika umri mdogo ni kukosa elimu pamoja na umasikini kwani familia nyingi ni duni.
Hahivyo, ametoa wito kwa wazazi kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi kwamba kama mtoto wa kike anaumri wa miaka 18 kushuka chini haruhusiwi kuozwa huku akiwataka wazazi hao kuwasomesha watoto na kuwasimamia katika maadili ili waweze kutimiza ndoto zao.
Comments
Post a Comment