BARAZA LA BIASHARA CHAMWINO LASISITIZA UWEKEZAJI


Na. Mwandishi Wetu, CHAMWINO

Baraza la biashara limefanya kikao kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, ikiwa na lengo la kukutanisha sekta ya umma na sekta binafsi ili kuboresha mazingira ya biashara wilayani hapa.
 
Mjumbe akichangia katika Baraza la Biashara Wilaya ya Chamwino
Wajumbe wa baraza hilo wametoa wito kwa wafanyabiashara wa nje na ndani ya wilaya ya Chamwino kuchangamkia fursa za kiuchumi zilizopo wilayani hapa na Dodoma kuwa makao makuu ya nchi kufanya uwekezaji wa viwanda vidogo, vya kati na vikubwa.

Akizungumza katika baraza hilo, Mwenyekiti mwenza wa baraza hilo, Richard Mmasi alisema kuwa zipo fursa za nyingi uwekezaji ikiwa ni pamoja na kilimo cha zabibu na mazao mengine, mifugo na madini.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya chamwino, Juliana Kilasara alieleza kuwa ni wakati sahihi kwa baraza kujipanga kutoa elimu kwa wanyabiashara ngazi ya vijiji na Kata ili kuwapa fursa ya kuwasilisha changamoto zinazowakabili ili serikali iendelee kuweka mazingira wezeshi kwa wafanyabiasha.

Nae Meneja wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Wilaya ya Chamwino, Omari Rajabu alitoa wito kwa wafanyabiasha na wananchi wanaostahili kulipa kodi ya majengo ambayo ni shilingi 10,000 kila mwaka.

Baraza la biashara la Wilaya lililenga kuwakutanisha viongozi wakuu wa Wilaya kutoka sekta binafsi na serikali chini ya usimamizi wa Mkuu wa Wilaya, kujadiliana jinsi ya kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini kwaajili ya kukuza uchumi kutumia sekta binafsi.
Malengo mengine ni kutengeneza mazingira bora ya kufanya biashara na uwekezaji, kuibua fursa za uwekezaji na kuzinadi fursa hizo kupitia kongamano za uwekezaji.

Chanzo: Tovuti ya wilaya


Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.