*YALIYOJIRI WAKATI WA MKUTANO WA MKUU WA MKOA WA MWANZA MHE. JOHN MONGELLA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA 58 YA UHURU LEO NOVEMBA 27, 2019 JIJINI MWANZA*
# Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi
kwenye maadhimisho ya sherehe za miaka 58 ya Uhuru na Miaka 57 ya
Jamhuri
# Maadhimisho hayo
yatafanyika Kitaifa Mkoani Mwanza tarehe 9 Disemba, katika Viwanja vya CCM
Kirumba
# Kauli mbiu ya
Sherehe hizo ni; Miaka 58 ya Uhuru na Miaka 57 ya Jamhuri:Uzalendo, Uwajibikaji
na Ubunifu ni Msingi wa Ujenzi wa Uchumi wa Taifa "
# Sherehe hizi
zinafanyika Kitaifa kwa mara ya kwanza Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza
#Maadhimisho
yatapambwa na vikundi vya Burudani wakiwemo Wasanii wa Kizazi kipya na Ngoma za
asili kutoka mikoa ya Mwanza, Kagera na Mara.
#Baadhi ya viongozi
wanaotarajiwa kuhudhuria Sherehe hizi ni pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi na Waziri Mkuu Mhe.
Kassim Majaliwa
#Viongozi
wastaafu wakiwemo Marais,Makamu wa Rais na Mawaziri wanaotarajiwa
kuhudhuria
# Wakuu wa Mikoa na
Viongozi mbalimbali wa mikoa ya Kanda ya Ziwa watashiriki katika kufanikisha
maandalizi ya Sherehe hizi
#Juma la kilele cha
maadhimisho haya litakuwa na shughuli mbalimbali zitakazofanyika kikanda
kuanzia Disemba 2, 2019 hadi tarehe 8,Disemba 8, 2019 katika mikoa ya Kagera,
Mara, Geita, Simiyu, Shinyanga na Mwanza
# Shughuli za Kikanda
zilizoandaliwa na mkoa wa Mwanza ni pamoja na Kongamano la Wanafunzi wa
vyuo vya Elimu ya Juu litakalofanyika Disemba 6, 2019 Chuo Kikuu cha
Mtakatifu Agustino Mwanza
# Shughuli nyingine
zitakazofanyika ni pamoja na mechi ya mpira wa miguu, Mchezo wa bao,
Mpira wa Kikapu, Pete na Volleball,Mashindano ya mbio za Mitumbwi, Ngonjera,
Maigizo,Kwaya na Mashairi.
*Imeandaliwa na Idara
ya Habari MAELEZO*
Comments
Post a Comment