Wauguzi wa wodi namba tatu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) waadhimisha utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa waliolazwa katika wodi hiyo kwa kutoa msaada wa dawa kwa wagonjwa wasiokuwa na uwezo wa kulipia gharama za matibabu

Mkuu wa Kitengo cha Ubora wa Huduma za Afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Tulizo Shemu akiwaeleza  wauguzi wa wodi namba tatu  jinsi ya kuwahudumia wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa moyo  ili waweze kujikinga na maambukizi (infection) kwenye eneo ambalo limefanyiwa upasuaji (kidonda) wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa  waliolazwa katika wodi hiyo

Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Huduma ya Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Mallya akiwapongeza wauguzi wa wodi namba tatu kwa upendo waliokuwa nao  kwa wagonjwa wanaowahudumia  wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa waliolazwa  katika wodi hiyo

Msimamizi wa wodi namba ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye pia ni Afisa Uuguzi Anastazia Moshi akieleza namna wauguzi wa wodi hiyo wanavyofanya kazi ya kuwahudumia  wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa waliolazwa  katika Taasisi hiyo

Maafisa Uuguzi wa wodi namba wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Ubora wa Huduma za Afya Dkt. Tulizo Shemu na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Huduma za Uuguzi Robert Mallya wakimkabidhi dawa zilizotolewa na wauguzi wa wodi hiyo Mkuu wa kitengo cha Ustawi wa Jamii Asha Salum kwa ajili ya wagonjwa wasiokuwa na uwezo wa kulipia gharama za matibabu wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa waliolazwa katika wodi hiyo.

Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Huduma za Uuguzi Robert Mallya, Mkuu wa Kitengo cha Ubora wa Huduma za Afya Dkt. Tulizo Shemu na Mkuu wa kitengo cha Ustawi wa Jamii Asha Salum wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete wakiwaongoza wauguzi wa wodi namba tatu kukata keki ikiwa ni ishara ya kuonesha upendo kati yao na wagonjwa wanaowahudumia wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa waliolazwa katika wodi hiyo

Afisa Uuguzi wa wodi namba tatu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jumaa Omary akimlisha keki mgonjwa aliyelazwa katika wodi hiyo ikiwa ni  ishara ya kuonesha upendo kwa wagonjwa wanaowahudumia wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa waliolazwa  katika wodi hiyo

Maafisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Huduma za Uuguzi wa Taasisi hiyo  Robert Mallya (aliyevaa safari suti) mara baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya kuadhimisha utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa waliolazwa katika wodi namba tatu

Maafisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Huduma za Uuguzi wa Taasisi hiyo  Robert Mallya (aliyevaa safari suti) mara baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya kuadhimisha utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa waliolazwa katika wodi namba tatu

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.