Na Jackline Victor Kuwanda, DODOMA
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Ashatu Kijaji amewataka wahitimu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo vijijini
kwenda kutumia maarifa na ujuzi walioupata wakati wakiwa chuoni, kuchangamkia
fursa zilizopo katika kujiajiri na kuzalisha ajira kwa vijana na
watanzania wote kwa ujumla.
Dkt. Kijaji ameyasema hayo jijini Dodoma
katika mahafali ya 33 ya chuo hicho kampasi kuu ya Dodoma kwa mwaka 2019.
Aidha, ameongeza kuwa Serikali itaendelea
kuboresha mazingira ya upatikanaji wa mitaji kwa vijana kupitia bajeti za Halmashauri,
benki ya maandeleo ya kilimo, asasi za kifedha pamoja na benki za biashara
nchini.
Naibu Waziri ametoa maelekezo kwa uongozi
wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kuongeza juhudi kwenye eneo la
utafiti kwa sababu bila utafiti hakuna mamlaka ya kusema wala kushauri chochote
mbele ya uso wa Tanzania na Dunia nzima kwa ujumla.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Mipango
Prof. Hozen Mayaya amesema chuo kimekuwa kikitoa mchango mkubwa kwa jamii
ambapo watumishi kutoka zaidi ya Taasisi mia mbili kutoka Serikali kuu, Mamlaka
ya Serikali ya Mtaa, Mashirika ya Umma na taasisi binafsi wamepata mafunzo
mbalimbali kwa lengo la kuongeza ufanisi kwenye majukumu yao.
Nao wahitimu ambao wamehitimu katika chuo
hicho Wamezungumza kwa furaha kwa kuhitimu kwao huku wakisema kuwa yale ambayo
wameelekezwa kuyafanya huko wanako kwenda wataenda kuyafanyia kazi ikiwemo
suala la kujiajiri.
=30=
Comments
Post a Comment