Mwenyekiti wa Bodi ya
Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Stephen Wassira amesema Lengo la Chuo
hicho ni kuendelea kuwa kitovu Cha Msingi wa maadili ili vijana wanaomaliza
waweze kuwa viongozi bora katika Taifa.
Amesema hayo wakati wa
mahafali ya 14 yaliyofanyika chuoni hapo ambapo wahitimu zaidi ya Elfu Tatu
wametunukiwa Shahada zao.
Wassira amewataka
wahitimu kuwa mfano wa kuigwa katika jamii kutokana na matendo yao na pia kuwa
mabalozi wazuri ambao wanakiwakilisha vyema chuo katika Jamii zinaowazunguka.
“ Nendeni mkawe
mabalozi wazuri katika Jamii na pia mkajitofautishe na wanafunzi waliomaliza
katika vyuo vingine kutokana na maadili na nidhamu ambayo
mmejengewa hapa chuoni” amesema Wassira ambaye ni Mwenyekiti wa
bodi na mgeni rasmi wa mahafali hayo ya 14.
Amesema kuwa matendo
ya vijana waliosoma Chuo Cha Mwalimu Nyerere yatatafsriwa katika Jamii
kuwa mmesoma Chuo chenye jina kubwa la Mwalimu Nyerere ambaye ni Baba wa Taifa
la Tanzania.
Wassira amewataka
vijana hao kuhakikisha wanafanya kazi kwa juhudi na maarifa kwa lengo la
kuondoka na umasinini na kuwa umasikini hauwezi kuondoka kama uchumi wetu
haukui, huku akibainisha kuwa upo uchumi wa mtu mmoja mmoja na upo uchumi wa
nchi.
Kwa upande wake Mkuu
wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Shadrack Mwakalila amesema dira
ya Chuo hicho ni kuwa kitovu cha utoaji wa maarifa bora kwa kutoa Elimu
na mafunzo kuhusu ubunifu na uvumbuzi na kuendeleza amani na umoja wa kitaifa.
Prof. Mwakalila pia
ametaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana chuoni hapo kuwa ni pamoja na
Kuboresha mazingira ya
kufundishia, Kuongeza vitabu kwa kampasi zote na kuongeza udahili wa wanafunzi
ambapo kwa sasa kwa kampasi zote mbili idadi ya wanafunzi imefikia 9,796.
Mkuu huyo wa Chuo
ametaja mafanikio mengine kuwa ni pamoja na kukamilisha ujenzi wa ukumbi wa
mihadhara wenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 300 kwa mara moja, ufungaji wa
vifaa vya kisasa vya kufundishia, idadi ya watumishi imeongezeka kutoka 230 kwa
mwaka 2018 hadi kufikia 274, na idadi ya walimu imeongezeka kutoka 193 katika
mwaka 2018 hadi 210 kwa mwaka 2019.
Imetolewa na:
Kitengo Cha Habari na
Mawasiliano,
Chuo Cha Kumbukumbu ya
Mwalimu Nyerere
29/11/2019
![]() |
Maandamano ya Wahitimu katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere |
![]() |
Wahitimu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere wakiwa wameinua kofia zao juu |
Comments
Post a Comment