Na Jackline Kuwanda,Dodoma.
Mkazi wa eneo la kisasa jijini Dodoma
Bwana Saimon Mapunda Jumbe (43) anayejishughulisha na kazi za fundi
ujenzi anashikiliwa na Taasisi ya kuzua na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoni
hapa kwa kosa la kujifanya Afisa wa Takukuru kinyume na kifungu cha 36
cha sheria ya kuzuia na kupambana Rushwa sura 329 marejeo ya mwaka 2018.
Bwana Simon Mapunda Jumbe Mkazi wa kisasa jijini Dodoma |
Mtuhumiwa huyo amekuwa akijfanya Afisa
Takukuru kwa kuwalaghai watu na kudai fedha akisingizia kwamba atawasiadia
kupata ajira TAKUKURU na ofisi zingine za serikali.
Akizungumza leo na Waandishi wa habari ,
Mkuu wa TAKUKURU Mkoani hapa Sosthenes Kibwengo amesema kuwa uchunguzi wao
umebaini kuwa mtuhumiwa amekuwa akifanya utapeli katika maeneo mengi na kutumia
mbinu mbalimbali .
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma Sosthenes Kibwengo |
‘’ katikati ya mwezi april mwaka,
tulipokea taarifa kwamba mtuhumiwa Bwana Jumbe anajiita Afisa Takukuru Mkoa wa
Dodoma ,ufuatiliaji wetu umeonesha kwamba mtuhumiwa aliwaahidi kaka wa mtoa
taarifa wetu kazi ya udereva ndani ya takukuru na baada ya mtu huyo kumweleza
kwamba hana leseni ya udereva daraja c ndipo mtuhumiwa akataka apewa shilingi
laki tatu na hamsini (350,000) ili amsaidie kupata leseni baada ya kupokea
taarifa hii na sisi tukaweka mtego na kumnasa mtuhumiwa akiwa eneo la kisasa
jijini Dodoma tarehe 14/4/2020’’ Alisema’’ kibwengo
Katika hatua nyingine , amesema kuwa
TAKUKURU inawashikilia watu watatu kwa makosa ya kuomba na kupokea Rushwa.
‘’Takukuru Mkoa wa Dodoma inapenda
kuufahamisha umma kuwa imeafikisha mahakama ya hakimu mkazi Dodoma kuwafungulia
shauri la jinai Na.80/2020 watu watatu ambao ni Bwana Chizenga Masagasi Chimya
(56) ambaye ni afisa mtendaji wa kijiji cha muungano wilaya ya chamwino na Bwana
Salehe Wistone Chagulula (45) makosa ya kuomba na kupokea hongo ya shilingi
elfu sabini pamoja na Bwana Jonas ivan Nganje (48) ambaye mwenyekiti wa
kitongoji cha iyoyo naye atafikishwa mahakamani kwa kosa la kushawishi na
kupokea shilingi elfu ishirini na tano (25,000) kwa mtoa taarifa ‘’ Kibwengo
Akizungumzia agizo la serikali la
kufuatilia Madeni ya vyama vya ushirika ,kwa kipindi cha April ,2020, amesema
TAKUKURU Dodoma imefanikiwa kurejesha shilingi milioni hamsini na saba,laki
tano sitini na sita elfu miambili thelathini na mbili na senti hamsini (57,566,232.50)
kutoka kwa viongozi wanachama 41 wa vyama sita vya akiba na mikopo (SACCOS)
husika zinazostahili.
‘’kutokana na takwimu hizo hadi sasa
Takukuru mkoa wa Dodoma tumeokoa jumla ya shilling milioni mia moja tisini na
nne na wiki ijayo kwa kushirikiana na Mrajis Msaidizi wa vyama vya ushirika
tukakabidhi fedha hizo kwa saccos husika zinazostahili’’ Kibwengo
Hatahivyo, amekikumbusha Chama cha
walimu (CWT) ambao wanaendelea na chaguzi zao mkoani hapa kujiepusha na
vitendo vya rushwa na kwamba wataendelea kufuatilia chaguzi hizo na kuwahoji na
kuwachukulia hatua stahiki wale wote wanaothibitika kujihusisha na vitendo vya
rushwa bila kujali nafasi zao.
‘’cha msingi wote wanatakiwa
kuzingatia mwongozo na taratibu za chama nan chi katika chaguzi hizo kujiepusha
na vitendo vya rushwa hii ni pamoja na wale wote wanahojiwa na
Takukuru,tunawataka mara moja tabia ya kutoa taarifa za chunguzi zetu kwani
hilo ni kosa kwa mujibu wa sheria na hatua stahiki zitachukuliwa kwa wote
wakatakao bainika’’ Kibwengo
Comments
Post a Comment